Mlima kilimanjaro ni mlima mrefu kupita yote hapa barani AfriKa, ni mlima wa kipekee kwani sio rahisi kukuta barafu katika ukanda wa kitropiki, lakini mlima kilimanjaro una barafu iliyo tambaa kwenye kilele chake mita kadha wa kadha na kufanya kiwe kivutio kikubwa cha watalii hapa Tanzania. Ndugu msomaji wangu wa blog hii, napenda kuku habarisha kwamba upekee wake pia ni pamoja na kuwa mlima ulio simama pekee yake bila kuwa na milima saidizi.
Mlima Kilimanjaro una urefu wa mita 5895 ambao uko kwenye uwanda wa bonde la milima ya mashariki.
mlima kilimanjaro |
FATILIA MFULULIZO WA MAKALA HII
Jina la Kilimanjaro halija julikana nini hasa chanzo chake, lakini kwa tafiti
nilizo zifanya neno hilo inasemekena kwamba kuna mchunguzi wa bara la Ulaya alilipata
neno hilo mnamo mwaka 1860 na akaliripoti kuwa ni neno la kiswahili. Lakini
chanzo kingine kiliona neno Kilimanjaro ni kilima-njaro. Kuna mtafiti mwingine
aliye julikana kwa jina la Johann Krapf yeye alisema kuwa ni mlima wa wamkubwa, au mlima wa karavani, kilima maana
mlima na Jaro akimaanisha karavani.
Kwa
hiyo nitaweza kusema kila mtu ana sema anavyo taka hasa hawa wakuja, ila
wenyeji wa mlima huu wachaga ambao wamezaliwa wakaukuta pale wanasemaje?
Tunajua kuwa kuna wachaga wa lafudhi tofauti tofauti, hii pia ina sadikika ndio
chanzo jina Kilimanjaro liwe na utata juu ya maana yake. Wengine wanadai kuwa
ni mlima mweupe, ambapo njaro ni weupe kama ilivyo tumika hapo awali, au
wengine wanasema njaro ni mmang’ao, neon hili tunalipata katika makabila
tofauti tofauti kwamfano neno njaro kwa kabila la wakamba aliandika Krapf kwamba
alikuwa Jagga na aliona Kima jajeu, mlima mweupe(Kiima kyeu) ambapo neno
Kilimanjaro likaanza kutumika kwa watafiti wengi.
Lakini
hatu ishii hapo tu, tukienda mbali zaidi, wengine wanadai kuwa ni neno la
Kiswahili. Kilima, tatizo lina kikuja kuwa Kilima ni hill kwa kingereza.
Tukumbuke kwamba wazungu walipokuja Tanzania walikuwa hawajui lugha yetu
hadhimu ya Kiswahili, wakabadilisha
mlima kwenda kilima kwa msemo jina la wa wachagga, Kibo na Mawenzi.
Ndugu
msomaji wa makala hii, tukienda mbali zaidi Kileman
sehemu ya mlima Kilimanjaro limetokana na neno Kileme likimaanisha pigwa/tekwa
au Kilelema imekuwa ngumu au kushindikana. Jaro sehemu ya neno limenymbuliwa
kwenye neno Njaare, ndege au chui
hususani jyaro karavani
Nisikuchoshe
mpenzi msomaji ilikutaka kujua hasa ukweli wa neno Kilimanjaro, sikuishihapo nlienda
mpaka uchaggani na kukutana na wazee wa Kichagga wanasema nini juu ya jambo
hili,
Hapo
zamani wachagga waliona mkusanyiko wa barafu, na wakaona ni vema kwenda
kuchunguza nini hasa, lakini hawakufanikiwa kufika, ndipo sasa wakaja na msemo
Kilemanjaare au Kilemanyaro au Kilelemanjaare wakimaanisha tumeshindwa,
haiwezekani, ndege, chui, au karavani. Kwahiyo imebaki dhahania tu, sasa watu
wa pwani kama wabeba mizingo walivyo kuja na wazungu walisikia wachagga wakisema
kilelenjaare au kilemajyaro, kwa maana rahisi haiwezekani kuupanda mlima huu,
ndipo sasa watu wa pwani waka watafsiria wazungu wakilihusisha na neno lao
Kilima. Kiswahili kilipo sanifishwa waliona nivema kusawazisha na kuita
Kilimanjaro.
Mlima
Kilimanjaro ukawa sehemu ya miliki ya Wajerumani kipindi cha ukoloni na kwa
lugha yao wakita Kilima Ndscharo.
Kilelekirefu ni kibo ambacho alifika mjerumani mmoja mwaka 1889, nakukiata Kaiser-Wilhelm-Spitze
mlima mrefu wa ngome ya Ujerumani, tulipo pata uhuru kilele kikabadilishwa jina
na kuitwa kilele cha Uhuru.
Imeandikwa na Fredy Michael
No comments:
Post a Comment