Viongozi
wa CDEA wakiwa na Mabalozi wa kampeni ya kupanda Mlima Kilimajaro wakat
wakizungumza na waandishi wa habari, kutoka kushoto ni Afisa wa
Program, Naamala Samson, Mkurugenzi Mtendaji wa CDEA, Ayeta Wangusa,
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya CDEA na balozi wa kampeni hiyo
Madaraka Nyerere, Mwanamuziki na balozi wa kampeni ya Kupanda Mlima,
Vitali Maembe, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya CDEA, Rose Mwalimu na
Afisa Habari wa CDEA, Mandolin Kahindi
Madaraka Nyerere, Mtoto wa Hayati Baba wa TaifaJulius Nyerere, pamoja na Mwanamuziki Mzalendo Vitali Maembe wameteuliwa na
shirika lisilo la kiserikali Culture and Development East Africa (CDEA) kuwa mabalozi
wa kushiriki kampeni ya kupanda Mlima Kilimanjaro ili kuhamasisha jamii
kuchangia ujenzi wa jukwaa la sanaa na ubunifu jijini Dar es Salaam.
Kampeni hiyo ya kupanda Mlima Kilimanjaro
imeandaliwa na CDEA kupitia njia ya kupanda Mlima Kilimanjaro kuanzia Septemba
7 hadi 13 mwaka huu ili kujenga jukwaa na sanaa na ubunifu litakalowapa fursa
wasanii na vijana kukutana, kufikiri na kubuni kwa pamoja ambapo mawazo ya kisayansi
yatakutana na sanaa na pia sanaa kukutana na taaluma nyinginezo nyingi.
Mkurugenzi Mtendaji wa CDEA, Ayeta Wangusa anasema “ili
kufanikisha kampeni yetu ya mwaka mmoja tuliyoipa jina la ‘FUN FOR FUNDS’, tumeona ni vyema kupanda mlima Kilimanjaro kwa kumtumia Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya CDEA, Madaraka Nyerere pamoja na Vitalis
Maembe ambaye ni mwanamuziki mzalendo”
Wangusa anasema fedha zitakazopatikana kwenye kampeni
hii maalumu zitatumika kusaidia uzalishaji wa kazi za ubunifu za njia mbalimbali
za mawasiliano-bunifu, kuwekeza katika kuanzisha maabara ya Filamu(yaani film lab) na kuchangia gharama za
uendeshaji wa shughuli za Jukwaa la sanaa na ubunifu.
Kwa upande wake Madaraka Nyerere anasema, “Nimekuwa
nikipanda Mlima Kilimanjaro mara kwa mara kwa lengo la kuchangia ujenzi wa
shule na shughuli nyinginezo za maendeleo, hivyo mwaka huu nimeona nifanye
jambo hili kuhamasisha uchangiaji wa jukwaa hili la sanaa na ubunifu kwa
kushirikiana na CDEA”
Madaraka anawaomba wadau mbalimbali kujitokeza
kuchangia katika kampeni hii ili kufanikisha kufikiwa kwa lengo lake. “Wadau watakaopenda
kuunga mkono zoezi hili,wanaweza kutuma michango yao kwa njia zifuatazo: M-PESA: 0765544714, TIGOPESA: 0713160668 Au Benki: CRDB BANK PLC, Jina la Akaunti: CULTURE AND
DEVELOPMENT EAST AFRICA TZS ACC:
0150210421400, USD ACC: 0252210421400, SWIFTCODE: CORUTZTZ”
Kwa upande wake Mzee wa ‘Sumu ya Teja’, Vitali Maembe anasema pamoja na kuwa hii ni mara ya
kwanza kupanda Mlima Kilimanjaro amefanya mazoezi ya kutosha kumuwezesha kufika
kwenye kilele jambo ambalo ni ndoto yake kubwa kama mwanamapinduzi wa kimuziki.
Culture and Development East Africa (CDEA) ni shirika lisilo la
kiserikali linalotoa huduma kwa wasanii, viongozi wa utamaduni, wajasiliamali, maafisa
utamaduni na mipango miji. Pia hufanya kazi na Mashirika makubwa ya kimaendeleo,
taasisi za kiraia na Elimu katika maendeleo ya utamaduni, mipango na utekelezaji
kwa Tanzania na Ukanda wa Afrika Mashariki kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment