Aina mpya ya Dinosaria imetambuliwa
kufuatia kupatikana kwa mifupa nchini Tanzania.
Mabaki hayo ya Dinosaria yaliyopewa
jina la - 'Rukwatitan Bisepultus' - yalipatikana katika korongo moja kwenye
eneo la Rukwa, kusini magharibi mwa nchi hiyo.
Inadhaniwa mnyama huyo aliyekuwa
akiishi kwa kula majani, aliishi karibu miaka mia moja iliyopita, na alikuwa na
uzito sawa na tembo kadhaa na alikuwa na miguu ya mbele yenye urefu wa mita
mbili.
Mnyama huyo ni aina ya Titanosaurus
-- ambao ni wakubwa, na wanaokula nyasi.
Mabaki ya wanyama aina hiyo mpaka
sasa yamepatikana katika maeneo ya Amerika ya Kusini, bara ambalo lilijitenga
kutoka Afrika katika kipindi cha Cretaceous, (kipindi ambacho miamba ya chokaa
iliumbika) takriban miaka milioni mia moja na arobaini iliyopita.
No comments:
Post a Comment